UTENGENEZAJI NA MATUMIZI YA MBOLEAVUNDE KATIKA KILIMO
UTENGENEZAJI NA MATUMIZI YA MBOLEAVUNDE KATIKA KILIMO
Mimea inapokuwa shambani hufyonza virutubisho vya mimea kutoka udongoni. Kati ya virutubisho hivyo, vilivyo muhimu zaidi ni nitrojeni, fosforasi, potasi, kalisi na feri. Mimea hutumia virutubisho hivyo kwa kukua, ku…
About This Content
Mimea inapokuwa shambani hufyonza virutubisho vya mimea kutoka udongoni. Kati ya virutubisho hivyo, vilivyo muhimu zaidi ni nitrojeni, fosforasi, potasi, kalisi na feri. Mimea hutumia virutubisho hivyo kwa kukua, kuzaa, kujiimarisha na kupevusha matunda ili kutupatia mavuno yaliyo mengi na bora. Karibu sehemu zote za mimea zina virutubisho. Sehemu hizo ni mizizi, mashina, majani, maua na matunda. Lakini, si sehemu zote hizo hutumiwa na binadamu kwa chakula. Kwa kawaida sehemu zinazotumiwa ni maua, majani, mbegu matunda au tyuba. Hata hivyo, sehemu halisi inayotumika hutegemea aina ya zao au mmea. Sehemu zinazobaki ambazo hazitumiwi na binadamu au mifugo kwa chakula hubaki na virutubisho hivyo. Iwapo sehemu kama hizo zitaachwa ziharibike ovyo huko shambani, au kuzichoma moto, hasa nje ya shamba, aina hizo za vyakula zitapotea bure bila kuwafaidia wakulima wala taifa. Njia ya kuhakikisha kwamba masalia hayo ya mimea yanawafaidia wakulima ni kuyarudisha udongoni. Njia iliyo bora ya kufanya hivyo ni kuyaozesha masalia ya mimea na kuyatumia kutengeneza mboleavunde. Vivyo hivyo kwa masalia ya wanyama (hasa mifugo). Wanyama hula mimea. Kiasi cha chakula hicho hutumiwa na wanyama hao kwa kukua, kuzaa, kufanya kazi na kuishi. Kiasi kilichobaki hutolewa nje kama kinyesi. Kinyesi hicho kina virutubisho muhimu vya mimea. Njia nzuri ya kutumia kinyesi hicho cha mifugo ni kukitumia kutengeneza samadi na mboleavunde na kuziweka udongoni ili kustawisha mazao. Kufanya hivyo ni kudumisha uhai wa udongo na viumbehai vingine. Kitabu hiki kinahusu namna ya kutengeneza mboleavunde iliyo nzuri na jinsi ya kuitumia shambani. Kitabu kimetengwa katika sura zifuatazo: Sura ya kwanza inatoa maelezo mafupi kuhusu udongo ambao ni moja ya nguzo kuu za kilimo. Sura ya pili inahusu mbolea kwa jumla. Sura ya tatu inaeleza sababu ya kutumia masalia ya mimea na wanyama kutengeneza mboleavunde. Sura ya nne inahusu misingi ya utengenezaji wa mboleavunde. Sura ya tano inahusu njia kuu za kutengeneza mboleavunde. Sura ya sita inaeleza kwa muhtasari, sifa, faida na matumizi ya mboleavunde. Ni matumaini yangu kuwa Wasomaji watakitumia kitabu hiki ili kuendeleza kilimo cha kutumia mboleavunde nchini. Istlahi zilizotumika katika kitabu ni zile zilizosanifiwa na Baraza la Kiswahili la Taifa.
Publication Details
| Category | Agriculture |
| Publisher | TEPU |
| ISBN | 978-9976-98-217-6 |
| Publication Year | 2026 |
| Pages | 72 |
| Chapters | 6 |
| Language | Swahili |
| Academic | No |
| Visibility | Public |
| Formats |
Reading Access
Purchase or subscribe to unlock this content.
Open Reader