ELM-DIGITAL LIBRARY
Book

Silaha 100 za Kiongozi

by Pius B. Ngeze
Book Purchase + Subscription 2500 TZS
Silaha 100 za Kiongozi
Type Book
Access Purchase + Subscription
Language Swahili
Published Aug 07, 2026

Silaha 100 za Kiongozi

by Pius B. Ngeze
Book Purchase + Subscription 2500 TZS

Silaha 100 za Kiongozi, ni silaha za aina ya pekee na ni za lazima kwa kila kiongozi. Hizi ni tofauti kabisa na silaha tulizozoea kuziona au kuzisikia. Silaha hizi zimetengenezwa ili zimsaidie kiongozi kumlinda dhidi ya…

About This Content

Silaha 100 za Kiongozi, ni silaha za aina ya pekee na ni za lazima kwa kila kiongozi. Hizi ni tofauti kabisa na silaha tulizozoea kuziona au kuzisikia. Silaha hizi zimetengenezwa ili zimsaidie kiongozi kumlinda dhidi ya mashambulizi kutoka kwa “maadui” wake. Katika kitabu hiki, neno Kiongozi, linajumlisha viongozi wa famil ia, siasa, serikali, dini, kazi, ushirika, taasisi za serikali, asasi zisizo za serikali, asasi za serikali, mashirika ya umma, makampuni na wengine. Viongozi hawa wote wanapigwa vita vya kila namna, kwa hiyo, ili waendelee kuongoza wanahitaji kuwa na silaha za kujilinda. Vita hivi vinatoka kwa viongozi wenzao, kwa watu wanaowaongoza na hata watu wasiowaongoza. Vita vipo na ni vya kweli. Asipopigana kwa kutumia silaha hizi ataan gamia. Wananchi nao (watu wasio viongozi) wanahitaji kujua silaha hizi ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya viongozi wao. Wakizijua watakuwa wameelewa mambo ya kutegemea kutoka kwa viongozi wao. Mtengenezaji wa silaha hizi, Ndugu Pius Bakengera Ngeze (pichani), ana uzoefu wa miaka mingi akiwa kiongozi wa familia yake, kiongozi kazini na kiongozi wa siasa nchini. Kwa sababu hii, ametengeneza silaha hizi kutokana na uzoefu alionao katika uongozi. Kitabu hiki ni cha lazima na muhimu kwa kila kiongozi na kila mwananchi. Aidha, kitabu chenyewe ni silaha, kwa maana kimehifadhi Silaha 100 za Kiongozi. Kinunue, kisome na kutafakari kwa makini silaha hizi na kuzitumia.

Publication Details

Category Siasa
Publisher TEPU
ISBN 978-9987-07-005-3
Publication Year 2026
Pages 115
Chapters 100
Language Swahili
Keywords Silaha 100 za kiongozi
Academic Yes
Visibility Public
Formats PDF

Reading Access

Purchase or subscribe to unlock this content.

Open Reader

Share & engage

No ratings yet — be the first.
Your rating
Comments

No comments yet.

Report this content