ELM-DIGITAL LIBRARY
Book

Sheria ya Ardhi Tanzania Umilikaji na Matumizi

by Al-Muswadiku K. Chamani
Book Purchase + Subscription 2000 TZS
Sheria ya Ardhi Tanzania Umilikaji na Matumizi
Type Book
Access Purchase + Subscription
Language Swahili
Published Aug 06, 2026

Sheria ya Ardhi Tanzania Umilikaji na Matumizi

by Al-Muswadiku K. Chamani
Book Purchase + Subscription 2000 TZS

Mwandishi ambaye kwa taaluma ni Mwalimu, Mwanasheria na Mwandishi wa vitabu kadhaa wa siku nyingi ambaye pia ni Wakili wa kujitegemea, ametumia taaluma hizo kuwaelimisha wananchi juu ya utawala wa Sheria ya Ardhi Tanzan…

About This Content

Mwandishi ambaye kwa taaluma ni Mwalimu, Mwanasheria na Mwandishi wa vitabu kadhaa wa siku nyingi ambaye pia ni Wakili wa kujitegemea, ametumia taaluma hizo kuwaelimisha wananchi juu ya utawala wa Sheria ya Ardhi Tanzania. Nchini Tanzania, kuna sheria kuu mbili zinazohusu utawala wa ardhi, nazo ni Sheria ya Ardhi ya Vijiji, ambayo ni Sura 114 R.E. 2002 na Sheria ya Ardhi Tanzania ambayo ni Sura R.E. 2002. Sheria ya Ardhi inatumika katika maeneo ambayo yamesajiriwa rasmi na serikali, kwa mfano, maeneo ya mjini yenye hatimiliki, na kwa yasiyo na hatimiliki panatumika sheria ya mila. Mifano mingine ni maeneo yaliyohifadhiwa kama vile Hifadhi za Taifa, Misitu nakadhalika. Katika Sheria ya Ardhi Tanzania, zipo taratibu mbalimbali zinazoonyesha jinsi ya kumiliki ardhi mijini, sheria ya kupangisha, sheria ya dhamana, kuweka rehani ardhi iliyopimwa na isiyopimwa. Lakini, yapo mambo fulani ambayo yamo katika Sheria ya Ardhi ya Vijiji na pia katika Sheria ya Ardhi Tanzania. Kwa mfano, sheria ya mila inatumika kumiliki ardhi vijijini hata mijini. Sheria ya Ardhi ya Vijiji imeelezwa kwa undani katika kitabu kingine cha mwandishi huyu, kiitwacho Ufafanuzi wa Sheria ya Kumiliki Ardhi Vijijini Tanzania. Kwa kutumia Kiswahili rahisi, lakini, sanifu, amechambua na amefafanua sura mbalimbali 85 vya sheria hiyo, kama vinavyoonekana kwenye YALIYOMO. Amefanya kazi hiyo kwa kutumia njia ya maswali 106 na kuyatolea majibu. Katika kujibu hababaishi, maana, kama taaluma ya sheria inavyomtaka, ananukuu Hukumu 45 zilizotolewa na Majaji maarufu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania na wa Mahakama ya Rufaa ya Afrika Mashariki. Aidha, amerejea vitabu vya sheria 5 na sheria 21. Kitabu hiki ni cha msaada na cha lazima kwa viongozi wa ngazi zote na wananchi wote. Kukisoma kutapunguza wingi wa migogoro, dhuluma na malalamiko juu ya umilikaji wa ardhi nchini.

Publication Details

Category SHERIA ZA TANZANIA, UMILIKI WA ARIDHI NA HAKI ZA WANANCHI
Publisher TEPU
ISBN 978-9987-07-047-3
Date Published 2026-08-06
Publication Year 2018
Pages 160
Chapters 85
Language Swahili
Keywords ARDHI
Academic No
Visibility Public
Formats PDF

Reading Access

Purchase or subscribe to unlock this content.

Open Reader

Share & engage

No ratings yet — be the first.
Your rating
Comments

No comments yet.

Report this content