SAFARI NDEFU YA MAISHA YA MZEE CLEMENT KWEZI NSHERENGUZI
SAFARI NDEFU YA MAISHA YA MZEE CLEMENT KWEZI NSHERENGUZI
Kupitia kitabu hiki wasomaji wake watapata fursa ya kumwelewa zaidi Mzee Clement. Safari yake imekuwa ndefu na bado inaendelea.Safari yake haikuwa ya lami. Imekuwa ya misukosuko, milima na mabonde. Lakini, hakukata…
About This Content
Kupitia kitabu hiki wasomaji wake watapata fursa ya kumwelewa zaidi Mzee Clement. Safari yake imekuwa ndefu na bado inaendelea.Safari yake haikuwa ya lami. Imekuwa ya misukosuko, milima na mabonde. Lakini, hakukata tamaa, alipambana na kusonga mbele, hatimaye, ameibuka na ushindi. Kamwe hakukubali kushindwa. Ana historia ya kuthubutu, kujaribu na kuwa mwanaharakati.Kitabu hiki kina sehemu mbili: Sehemu ya Kwanza ameiandika mwenyewe. Sehemu ya Pili imeandikwa na watu mbalimbali waliotoa maoni yao jinsi wanavyomwelewa. Kwa kuyasoma utazidi kumwelewa zaidi Mzee Clement Kwezi Nsherenguzi. Maisha yake yanaweza kuwa shule kwa watu wengi. Tabia, misimamo ya maisha na hulka yake vimemsaidia kuishi kwa furaha wakati wote licha ya miiba na maumivu. Kitabu hiki kitawasaidia watu wengi kujifunza kuwa maisha ni mapambano na sharti tupambane ili tuwe washindi maishani.
Publication Details
| Category | WASIFU NA TAWASIFU WA WATU MASHUHURI WA KAGERA |
| Publisher | TEPU |
| ISBN | 978-9976-58-403-5 |
| Publication Year | 2023 |
| Pages | 163 |
| Chapters | 18 |
| Language | Swahili |
| Keywords | maisha |
| Academic | Yes |
| Visibility | Public |
| Formats |
Reading Access
Purchase or subscribe to unlock this content.
Open Reader