ELM-DIGITAL LIBRARY
Book

RITA KOKU

by Maria Ruhumuliza Paul
Book Purchase + Subscription 3000 TZS
RITA KOKU
Type Book
Access Purchase + Subscription
Language Swahili
Published Aug 06, 2026

RITA KOKU

by Maria Ruhumuliza Paul
Book Purchase + Subscription 3000 TZS

Rita Koku ni msichana mzuri mwenye umbo la kupendeza na pia alikuwa na tabia nzuri. Alikuwa ni kifungua mimba katika familia ya Bwana na Bibi Philipo. Kutokana na tabia yake nzuri wazazi wake walimpenda sana. Alifanikiw…

About This Content

Rita Koku ni msichana mzuri mwenye umbo la kupendeza na pia alikuwa na tabia nzuri. Alikuwa ni kifungua mimba katika familia ya Bwana na Bibi Philipo. Kutokana na tabia yake nzuri wazazi wake walimpenda sana. Alifanikiwa kusoma hadi kidato cha nne na kupata sifa za kuweza kujiunga na chuo cha ualimu. Lakini, Rita hakupenda kwenda Chuo hicho. Wazazi wake walimshawishi aende Chuoni ila Rita hakukubaliana nao. Wazazi wake walimkabidhi biashara ya Duka la Rejareja. Akiwa dukani hapo vijana wa aina mbalimbali walitumia nafasi hii kumtafuta Rita kimapenzi. Rita hakuwa msichana mwenye papara, hivyo, hakupenda kujirahisi kwa wanaume hao. Baadaye Rita aliamua kupendana na kijana aitwaye Leonard, kwa kifupi Lenny. Hatimaye, Lenny alimweleza Rita kwamba alitaka amuoe. Baada ya Rita kufikiri kwa siku kadhaa alimkubalia. Walipima UKIMWI na kukutwa hawana virusi vya ugonjwa huo. Rita alimweleza mama yake habari za kumpata mchumba. Lakini, mama yake hakukubaliana naye kwa sababu wazazi hawa walishamwandalia Rita mvulana wa kumuoa ambaye alikuwa bado yuko masomoni. Lakini, Rita alijichukulia uamuzi, akaolewa na Lenny baada ya kutoroshwa nyumbani kwao. Huko, Lenny hakutaka Rita atembelee majirani. Rita akiwa mjamzito, Lenny alipata safari na Rita alitumia muda huo kwenda kwa jirani yake Bi Amina ambaye alimjulisha kuwa Lenny alikuwa jambazi sugu. Ni nini kilimpata Rita ambaye anapata habari hizi akiwa mjamzito? Je, wazazi wa Rita wana hali gani baada ya Rita kutoroshwa nyumbani? Soma hadithi hii ya kusisimua uyajue haya.

Publication Details

Category Riwaya
Publisher TEPU
ISBN 978-9987-42-629-4
Date Published 2023-05-31
Publication Year 2023
Pages 63
Chapters 9
Language Swahili
Academic No
Visibility Public
Formats PDF

Reading Access

Purchase or subscribe to unlock this content.

Open Reader

Share & engage

No ratings yet — be the first.
Your rating
Comments

No comments yet.

Report this content