KISU KIKALI CHA MOYONI
KISU KIKALI CHA MOYONI
Kufunga ndoa ni kuingia katika kifungo cha maisha ambacho huwezi kutoka tena, kama kweli unataka ustawi wa kifamilia. Ndiyo maana unatakiwa kujitafakari vyema, kabla ya kujitosa katika maisha ya ndoa. Na ndoa ndoana ina…
About This Content
Kufunga ndoa ni kuingia katika kifungo cha maisha ambacho huwezi kutoka tena, kama kweli unataka ustawi wa kifamilia. Ndiyo maana unatakiwa kujitafakari vyema, kabla ya kujitosa katika maisha ya ndoa. Na ndoa ndoana inamaanisha kwamba samaki akishanasa kwenye ndoano, hawezi tena kurudishika majini kuendelea na maisha yake ya uhuru, baada ya kula chambo kitamu; kama wasemavyo Waswahili: penye urembo pana urimbo. Wengi wetu tumezoea kujisemea kwamba Darasa la Saba limetema vimwana vigori, twende tukajizolee tujiolee. Lakini, siku hizi elimu-msingi imesogezwa hadi Kidato cha Nne, ili watoto wa shule waendelee kulelewa na kukulia shuleni; kiasi kwamba ukiwaona wakikuchekea, utadhani ni wanawali tayari kwa kuolewa. Kumbe serikali imekwishaweka gharama kali ya pingu za maisha kwa wote wanaowaoa wanafunzi, na kujikalia kimya, labda kwa sera ya gusa unate; ikingoja mtu ajipendekeze! Ukitaka kufahamu jinsi watu wanavyopotezwa kwa kufungwa pingu za maisha, basi soma au tazama tamthiriya hii ya kimahaba.
Publication Details
| Category | Tamthiliya |
| Publisher | TEPU |
| ISBN | 978-9976-58-417-2 |
| Date Published | 2024-06-13 |
| Publication Year | 2024 |
| Pages | 58 |
| Chapters | 5 |
| Language | Swahili |
| Keywords | Hadithi, Riwaya, Mapenzi |
| Academic | Yes |
| Visibility | Public |
| Formats |
Reading Access
Purchase or subscribe to unlock this content.
Open Reader