ELM-DIGITAL LIBRARY
Book

Kilimobiashara na Kanuni za Kukifanikisha

by Pius B. Ngeze
Book Purchase + Subscription 3000 TZS
Kilimobiashara na Kanuni za Kukifanikisha
Type Book
Access Purchase + Subscription
Language Swahili
Published Aug 07, 2026

Kilimobiashara na Kanuni za Kukifanikisha

by Pius B. Ngeze
Book Purchase + Subscription 3000 TZS

Kilimo cha Mazoea au Kilimo cha Kujikimu ni kile ambacho ni cha hali duni sana, kwa ajili ya kupata chakula. Ni kilimo cha kutumia majembe ya mkono, bila utaalamu, mtaji kidogo au bila uwekezaji, kanuni za kilimo ch…

About This Content

Kilimo cha Mazoea au Kilimo cha Kujikimu ni kile ambacho ni cha hali duni sana, kwa ajili ya kupata chakula. Ni kilimo cha kutumia majembe ya mkono, bila utaalamu, mtaji kidogo au bila uwekezaji, kanuni za kilimo cha kisasa hazitumiki na kinategemea mvua zinazonyesha kwa msimu. Mbegu za kienyeji ndizo hutumika kila msimu na hutokana na mavuno ya msimu uliopita. Kwao mbegu za chotara hazijulikani. Ardhi inayotumika ni kidogo, mbolea za aina zote hazitumiki. Kutokana na kutokuwa na ujuzi na uwezo wa kununua viuatilifu, kiasi kikubwa cha mavuno hupotea na ubora wake hushuka sana kutokana na kushambuliwa na magugu, magonjwa, wadudu, ndege na wanyama waharibifu. Kutokuwa na maghala au stoo za kuhifadhia mavuno, upotevu ni mkubwa. Tija ya ardhi iko chini sana. Matokeo yake ni umaskini wa wakulima, ambao ndio wengi nchini, wa mwaka hadi mwaka. Hawana fedha za kununulia mahitaji mengine, kwa baadhi yao chakula hakiwatoshelezi kwa mwaka mzima na mchango wao kwa pato la taifa ni mdogo. Ili kutoka kwenye mkwamo huo wa wakulima wadogo ambao ndio wengi nchini, ni lazima kuanzisha Kilimobiashara. Kuanzishwa kwa kilimo hicho ni kuwekeza mtaji (kwenye kilimo hicho). Mtaji ni mgumu kupatikana kwa ajili ya kilimo, lakini, pakiwa na sera ya dhati ya chama tawala na serikali, utapatikana. Kwa kawaida, wanaanza watu wachache, lakini, idadi yao itaongezeka kila mwaka. Kilimobiashara ni mbadala wa kilimo cha mazoea ambacho hakina budi kipotee hapa nchini. Kilimobiashara ni Mapinduzi ya kilimo cha kujikimu. Kilimobiashara ndicho mkombozi wa wakulima wengi nchini. Kilimobiashara kinahitaji sera madhubuti ya serikali iliyodhamiria kuwakomboa wakulima wanyonge na kuinua uchumi wa taifa. Mkulima wa kilimobiashara ni Mwekezaji, Mjasiriamali, Mfanyabiashara na Mkulima-mfanyabiashara. Lengo lake ni kupata faida kutokana na ongezeko la mavuno na ongezeko la ubora wake yanapouzwa kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.

Publication Details

Category Agriculture
Publisher TEPU
ISBN 978-9987-58-421-9
Publication Year 2024
Pages 40
Chapters 6
Language Swahili
Keywords kanuni za kilimo
Academic No
Visibility Public
Formats PDF

Reading Access

Purchase or subscribe to unlock this content.

Open Reader

Share & engage

No ratings yet — be the first.
Your rating
Comments

No comments yet.

Report this content