ELM-DIGITAL LIBRARY
Book

KILIMO CHA UMWAGILIAJI

by Pius B. Ngeze
Book Purchase + Subscription 3000 TZS
KILIMO CHA UMWAGILIAJI
Type Book
Access Purchase + Subscription
Language Swahili
Published Aug 13, 2026

KILIMO CHA UMWAGILIAJI

by Pius B. Ngeze
Book Purchase + Subscription 3000 TZS

Mwaka 1974 kulitokea upungufu wa mazao muhimu ya chakula nchini. Upungufu huu ulitokea kwa sababu ya ukosefu wa mvua katika mikoa kadhaa katika msimu wa kilimo wa 1972/73 na hata msimu wa kilimo wa 1973/74. Taifa …

About This Content

Mwaka 1974 kulitokea upungufu wa mazao muhimu ya chakula nchini. Upungufu huu ulitokea kwa sababu ya ukosefu wa mvua katika mikoa kadhaa katika msimu wa kilimo wa 1972/73 na hata msimu wa kilimo wa 1973/74. Taifa lililazimika kuagiza mahindi, mchele na ngano kutoka nchi za nje kwa thamani ya shilingi milioni 935 (za wakati huo). Nafaka hizi zilikuwa za kutosheleza mahitaji ya wananchi hadi Septemba, 1975. Ukame huu pia ulisababisha malisho ya mifugo kukauka na kiasi cha mifugo kufa katika mikoa fulani. Kutokana na balaa hili Halmashauri Kuu ya TANU ya Taifa ilikutana Moshi mwezi Machi, 1974, kujadili kuhusu umwagiliaji maji mashambani. Baada ya kikao chake, Halmashauri Kuu iliagiza wananchi mara moja waanze kilimo cha kutumia maji ya kumwagilia mashamba kwa kutumia mito, maziwa na maji ya aina yoyote yanayoweza kutumiwa kwa kazi hiyo. Wito huu ulipokelewa na mikoa yote nchini na mipango ya kufufua na kutumia mifereji iliyokuwa ikitumika zamani, lakini wakati huo ilikuwa haitumiwi, ikaanza kutayarishwa. Uwezekano wa kutumia mito, maziwa, mabwawa n.k. ukaanza kuchunguzwa kwa haraka sana. Mabonde mazuri yakaanza kuchunguzwa ili yatumiwe kwa kilimo. Itakumbukwa kuwa siku za nyuma hatukutilia sana mkazo umwagiliaji maji mashambani. Tulitegemea mno mvua. Hata hivyo, umwagiliaji maji mashambani si mgeni nchini, maana taarifa zinazopatikana zinaonyesha kwamba, hata kabla ya Wazungu kuingia nchini wananchi wa Usambara, Pare, Usukumani, Tukuyu na mahali pengine, walitumia maji ya kumwagilia kwa kustawisha mazao yao. Kwa upande mwingine, si wakulima wote nchini wanaweza kutekeleza kilimo cha aina hii bila kutumia gharama kubwa kwa sababu wanaishi au mashamba yao yako mbali na mito, maziwa na mabwawa. Hivyo, bora tujifunze na tuelewe jinsi ya kutumia vizuri na kuhifadhi maji ya mvua yanapopatikana. Kuhifadhi misitu yetu ya asili na kuanzisha mingine ni njia mojawapo ya kuhifadhi maji ardhini. Katika kitabu hiki tutaona umuhimu wa maji katika maendeleo ya kilimo, njia mbalimbali za kupata maji kwa ajili ya kilimo, njia kadhaa zinazoweza kusababisha upotevu wa maji ardhini, jinsi ya kuhifadhi maji mashambani na mengineyo

Publication Details

Category Agriculture
Publisher TEPU
ISBN 978-9987-07-033-6
Publication Year 2023
Pages 29
Language Swahili
Keywords Umwagiliaji
Academic No
Visibility Public
Formats PDF

Reading Access

Purchase or subscribe to unlock this content.

Open Reader

Share & engage

No ratings yet — be the first.
Your rating
Comments

No comments yet.

Report this content