JIFUNZE KUSTAWISHA VIAZI MVIRINGO
JIFUNZE KUSTAWISHA VIAZI MVIRINGO
Katika kundi la mazao ya mizizi, viazi mviringo ni maarufu na vina umuhimu wa pekee. Ni zao la chakula na biashara katika nchi nyingi zilizoendelea na zinazoendelea. Zao hili ni moja ya mazao manne ya chakula yanayozali…
About This Content
Katika kundi la mazao ya mizizi, viazi mviringo ni maarufu na vina umuhimu wa pekee. Ni zao la chakula na biashara katika nchi nyingi zilizoendelea na zinazoendelea. Zao hili ni moja ya mazao manne ya chakula yanayozalishwa kwa wingi na kutumiwa na watu wengi sana duniani. Hustawi vizuri kwenye sehemu za miinuko, kati ya meta 1,300 na 2,700 juu ya usawa wa bahari. Kipindi cha kukomaa ni kati ya miezi mitatu na mitano. Mbali na utamu wa viazi mviringo, lakini mlaji hujipatia asilimia kubwa ya chakula chenye asili ya wanga. Aidha, vina kiasi cha kutosha cha protini, madini, vitamini na maji.Umaarufu wake unaongezeka kila kukicha. Watoto,vijana na watu wazima hupenda kula viazi mviringo kama chipsi, viazi vilivyopondwapondwa, viazi vilivyochemshwa n.k. “Chipsi na kuku”, “chipsi na mayai”, “chipsi na nyama” au “chipsi kavu” ni majina maarufu sana katika familia nyingi, migahawa, hoteli, mama lishe n.k. hasahasa kwa watoto, vijana na watu wasiokuwa na muda wa kusubiri vyakula vinavyochukua muda mrefu kuviandaa.
Publication Details
| Category | Kilimo |
| Publisher | TEPU |
| ISBN | 978-9987-67-187-8 |
| Date Published | 2026-08-07 |
| Publication Year | 2019 |
| Pages | 48 |
| Chapters | 8 |
| Language | Swahili |
| Keywords | VIAZI |
| Academic | Yes |
| Visibility | Public |
| Formats |
Reading Access
Purchase or subscribe to unlock this content.
Open Reader